BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu msanii wa filamu Nuru Nassor ‘Nora’ amesema kimya hicho kimemfanya arudi kwa kishindo kwa kuja na filamu inayokwenda kwa jina la I can’t ambayo tayari ipo sokoni.
Nora amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kuwa bize na mambo yake binafsi lakini pia kupata muda mzuri wa kuandaa filamu zake binafsi alizopanga kuzifanya kwa mwaka huu.
“Kimya kingi kina mshindo sasa ndio nimerudi baada ya kimya kirefu na filamu yangu mpya ya I can’t tayari ipo sokoni” alisema Nora.
Aliongeza kuwa filamu hiyo ni moto wa kuotea mbalimbali na kuwataka wapenzi wa filamu kujipatia nakala halisi ya filamu hiyo ili kuweza kujionea wenyewe ujio wake mpya ambapo anaamini filamu hiyo itafanya vizuri sana.
0 comments:
Post a Comment