MSANII wa filamu Esther
Flavian, amesema kuwa anakamirisha kazi yake
mpya inayokwenda kwa jina la ‘Pastor’s Wife’,
ambayo itakuwa sokoni wiki chache zijanzo.
Akizungumza kwa
njia ya simu, msanii huyo amesema kuwa huo ndiyo ujio wa mpya kwa mwaka
huu na kilichobaki katkika filamu hiyo ni kumalizia kuhariri ili
iweze kwenda sokoni.
Aliongeza kuwa
filamu hiyo itakuwa inahusu maisha ya mchugaji na mke wake
pindi wanapokuwa nyumbani hivyo ni stori ambayo inataeleza maisha halisi
yanavyokuwa kwa watu hao.
“Filamu iko tayari imekamilika hivyo nawasihi mashabiki wangu wakae
mkao wa kuipokea kwa sababu itakuwa na matukio mengi ya kusisimua ambayo
hayana mfano hivyo kazi kwao,” alisema.
Pia msanii huyo
amewaomba mashabiki wake wote watakao itazama kazi hiyo watoe maoni yao
ili kuweza kujua wapi wamekosea.
0 comments:
Post a Comment