MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya bongo, Nasib Abdul ‘Diamond’, amesema kuwa kwa sasa anafikiria kuimba nyimbo za taarabu baada ya kukosa mpinzani kwenye bongo fleva.
Alisema katika muziki wake hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango alichokuwa nacho kwani katika kuthibitisha hilo ndani ya nyimbo zake hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha.
Aliongeza kuwa kikubwa kinachomsukuma kufanya aina tofauti ya muziki ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho kwani hakuna kitu anachoweza kushindwa kutokana na uwezo aliyokuwa nao.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.
“Naweza kufanya aina mbalimbali ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watashituka sana,” alisema.
Hata hivyo alipoulizwa kama anatshirikiana na wasanii wakongwe wa nyimbo hizo za mipasho, alisema kuwa kwanza atasimama mwenyewe lakini baada muda ataweza kuwashirikisha wasanii wengine.
0 comments:
Post a Comment