Baada ya kuamua kuachia single yake mpya ya ‘TABIA GANI’ iliyomrudisha katika
ramani ya muziki, Lucas Mkenda ‘MR NICE’ ametibitisha kupitia millardayo.com
kwamba mialiko ya showz aliyoipata mpaka sasa ni zaidi ya mitano, na
kilichomshangaza zaidi mingi imetoka nje ya nchi.
Nchi zilizomualika Mr Nice ni Kenya, Rwanda na Burundi, na kwa upande wa
Tanzania amepata showz kadhaa za mikoani ila ameshindwa kuzikubali mpaka
atakapo itambulisha rasmi tabia gani kwa wakazi wa 88.4 Dar es salaam japo
tayari ana mialiko ya Songea, Mwanza na Arusha.
Sababu nyingine inayomfanya ashindwe kuikubali hiyo mialiko ni pamoja na
kusubiri mfungo wa kwaresma upite kwanza.
“mapokezi ya hii single yamekua makubwa na kunishangaza, kweli kila mtu
alikua anatamani kuona Mr Nice amerudi, nimekua nikipata simu nyingi wengi
wameisikia Club, mwingine wimbo wako ndio ringtone yangu sasa hivi, kwa hiyo
nimefurahi sana, najipanga tu kikazi, sasa hivi nina meneja zaidi ya mmoja,
nina personal manager wangu na kuna mwingine anashughulika na mambo ya masoko
tu, kuna mambo mengine ukiniuliza hata siyajui, hiyo ndio kazi yao”
http://millardayo.com/
0 comments:
Post a Comment