Mwimbaji
tkoa nyumba ya vipaji THT Mwasiti Almasi ‘Mwasti’amesema tangu aingie kwenye
industry ya bongo fava huu ni mwaka wake wa tano huku akiwa na jumla ya single
nane.
Mwasiti
amesema katika nyimbo zote hizo zinazijulikana, katika kumbukumbu zake miongoni
mwa nyimbo zilizomfanya kupata mialiko na show nyingi kuliko single zote ni
wimbo wa ‘Nalivua Pendo’.
Aliyasema
hayo kupitia kipindi cha Amplifier cha Millard Ayo kinachorushwa na Clods Fm.
“Millard hata nikifa kesho, kesho kutwa
Nalivua Pendo kiukweli ni namba moja kwangu, ilinifanya nikakaa kimya muda
mrefu sana na nikaendelea kupata hela, ina nipa showz mpaka kesho kutwa, japo
Hao, sio kisa pombe, na Souljah nayo japo watanzania hawajaielewa sana ila
zimechangia kunipa kipato”
Mwasiti
amethibitisha pia kwamba single yake ya nalivua pendo, imempa asilimia 95 ya show
zote alizowahi kufanya, ambapo ameitoa good news nyingine leo kwamba baada ya
kuwa kimya kwa miezi zaidi ya saba, leo katoa single yake mpya inaitwa Kisima
inayozungumzia mapenzi tu, amesimama kama mwanamke ambae amependa.
“kisima
ni sehemu ambayo mahaba hayaishi kama unavyojua kisimani ni sehemu ambayo mtu
anachota maji, ndio hivyo hivyo kwa kisima hiki mahaba hayaishi”
0 comments:
Post a Comment