![]() |
Raisi wa Masharobaro Bob Junior |
RAISI wa masharobaro , Bob
Junior, amebonga
kuwa ile video ya wimbo wake wa ‘Nichum’,
itakuwa hewani Jumatatu hii.
Akiongelea video hiyo msanii huyo alisema kuwa ni kazi ambayo
imechukua muda mrefu hadi kukamilika hivyo anaamini itafanya vizuri kwani
imetengenezwa katika ubora wa kimataifa tofauti na nyingine alizowahi kuzitoa
hapoa awali.
Junior alisema kuwa ndani ya kichupa hicho amemtumia msanii wa
filamu ‘Lulu’, ambaye naye ameonesha uwezo wa kupitiliza.
“Video ipo mashabiki
wangu wataanza kuitazama kupitia televisheni mbambali, na naamini kwamba
wataipokea vizuri kwa sababu ni kazi ambayo imeandaliwa katika kiwango cha
kimataifa, in short ni moto wa kuotea mbali” alisema.
0 comments:
Post a Comment