Raia mmoja aliyetambulika kwa jina la Rajabu Athumani, jana alihukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio maarufu kama mlegezo au Kata K.
Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ambayo kwa mujibu wa karani wa Mahakama hiyo ni ya ubakaji, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana.
“Mtu kuvaa suruali chini ya makalio ikiwa sio maadili yetu na tamaduni zetu Waafrika hasa kwenye shughuli za Serikali na kuonesha nguo zake za ndani, anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo,” alisema Hakimu Wilberforce Luhwago.
0 comments:
Post a Comment