Monday, February 27, 2012

Z-anto sasa ajipanga na Superstar


Baada ya ‘Kisiwa cha Malavidavi’ kufanya vizuri, Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo Z-Anto, amesema kuwa baada ya ngoma hiyo, sasa anatarajia kutoa kazi mpya inayokwenda kwa jina laSuper Star’.
Akichonga na Samber Junior ,kuhusiana na kimya cha Msanii huyo, ambapo amedai kuwa kazi yake hiyo anayotarajia kuiachia hivi karibuni itakuwa ni moto wa kuotea mbali.
Mbali na ujio wa kazi hiyo pia amedai kuwa mwaka huu hafikili kutoa albamu kwani anatakuwa akitoa ngoma moja moja ambazo anaamini zitasaidia kumuweka juu ukiachilia mbali albamu.

“Kazi ipo katika mikono yangu kwa sasa ni hiyo, lakini baada ya wiki mbili nitakuwa katika mchakato wa kuitolea video hivyo naamini mambo yataenda vizuri tu,” Alisema.

0 comments:

Post a Comment