Friday, February 24, 2012

BABY MADAHA AJIUNGA NA TMK HALISI


Baada ya kutangaza nia ya kutaka kuwa mbunge, Mwanadada zao la Bongo Star Search, Baby Madaha, amejiunga rasmi kwenye Kundi la TMK Wanaume Halisi ambalo linaongozwa na Juma Kassim Ally Kiroboro ‘Sir Nature’.
Kujiunga TMK kumethibitishwa na mwanadada huyo pamoja na kiongozi wa kundi hilo Juma  Nature.
Madaha alikiri kufanya kazi na kundi hilo na kuongeza kwamba mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi ndiyo maana ameungana na vichwa vya kiumeni.
Kwa upande wa Nature, alisema, “Baby Madaha ndiye first lady wa Halisi. Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi.”
Baada ya shindano la BSS kumalizika, Baby alifanya kazi mbalimbali ndani na nje ya nchi, na kutambulika zaidi baada ya kuachia ngoma yake ya Amore ambyo ilifanya vizuri.

0 comments:

Post a Comment