MSANII wa muziki wa kizazi kipya
Banana Zorro, amesema kuwa katika suala la mavazi, mara nyingi huwa
ananunua nguo zenye gharama kubwa ambapo suti zote anazomiliki kila moja
amenunua kwa shilingi laki 500,000.
Akizungumza na DarTalk, msanii
huyo alisema hana tatizo la fedha hivyo kutoa kiasi hicho cha pesa haoni
tatizo kwani anahitaji kupendeza muda wote.
Alisema huwa anafanya manunuzi ya
nguo kwa mwezi mara tatu, na kila anapoenda dukani hutumia shilingi
milioni 10, hadi kumaliza mahitaji yake yote ikiwa pamoja na yale ya
familia.
“Najipenda sana na ndiyo maana
navaa nguo za bei mbaya, siyo kwamba ninajisifia lakni huo ndo ukweli
uliyopo, unajua maisha haya ukiwa hutumii pesa huwezi kuendelea au
kufanya chochote cha maana,” alisema.
0 comments:
Post a Comment