Monday, February 27, 2012

Skyner: Najipanga kutoa movie yangu


MSANII wa ndani ya Bongo Movie Industry Skyner Ally ‘Skyner’, amesema kuwa baada ya kucheza filamu nyingi za wasanii wenzake sasa anajipanga kutoa filamu yake ambayo itakuwa na mastaa kibao wa tasnia hiyo.
Skyner alisema kuwa tayari ameshacheza filamu nyingi za kushirikishwa hivyo anaamini iwapo atasimama kuhahakikisha filamu yake inatoka itafanya vizuri sokoni.
Alisema filamu yake hiyo kwa sasa bado hajaipa jina kwani yupo katika mchakato wa kuangalia wasanii ambao wanaweza kucheza katika kiwango ambacho anahitaji ingawa wapo baadhi ya nyota ambao majina yao yapo kichwani.

“Nimecheza sana filamu za watu hasa ‘Ray’, lakini kwa sasa nahitaji kusimama mwenyewe na kuonesha uwezo wangu, ingawa naamini itakuwa nzuri kwa sababu najipaga kuifanya iwe ni moja kati ya kazi zitakazofanya vizuri kimataifa,” alisema Skyner.

0 comments:

Post a Comment