Tuesday, February 21, 2012

KTMA:WALIOIBA NYIMBO KUNYANG'NYWA TUZO


Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro imesema itamnyang'anya tuzo msanii atakayebainika kwamba wimbo uliompatia tuzo hizo aliuiga.
Kauli hiyo ilitolewa na mmoja wa wanakamati hao, Innocent Nganyagwa katika semina ya wanamuziki wanaowania tuzo hizo iliyofanyika Alhamisi jijini Dar es Salaam.
“Tukubaliane, tuzo zitatolewa, lakini baadae hata kama ni mwakani, kamati ikigundua kuwa msanii ‘ulicopy na ku-paste’ tutakunyang’anya tuzo, cheti kila kitu sijui upande wa pesa kama utakuwa ushazitumia au vipi,” alisema Nganyagwa. Kauli hiyo ya Nganyagwa ilitokana na maoni yaliyoolewa na muandaaji wa muziki Man Water kwamba kuwe na tuzo ya ubunifu.
Akifafanua kwenye suala la ubunifu Man Water alisema kuwepo kwa kipengele hicho kutasaidia kuibua maproduza wabunifu huku akitolea mfano wimbo wa Dushelele wa Ali Kiba ambao ameutengeneza yeye.
“Kuwe na tuzo ya Producer mbunifu, kwa sababu kuna wengine unaona kabisa kazi zao wameiba mahali, yani msanii na Producer wanakuwa wamecopy na kupaste kazi ya mtu Fulani… hivi hawa kwanini wasipewe adhabu kali, hata kama ya kufungiwa kwa miaka miwili ikibidi, mfano kama Dushelele ule ni ubunifu, hivi unaweza kuuweka kwenye mziki gani, ipo kama Rhumba kidogo, kisanola ya kina Koffie, na mahali popote unachezeka hata mtu akitaka kucheza kama taarab anaweza” alisema Man Water.
 Aidha Man Water aliwaomba waandaaji kufikiria kutoa tuzo ya msanii anayeshindanishwa mara nyingi kwenye tuzo hizo, maana ya kuwa katika tuzo hizo kuna kitu ambacho anacho hivyo basi waandaji watoe tuzo ya kutambua hilo.

0 comments:

Post a Comment