Tuesday, February 21, 2012

BABY MADAHA AJIPANGA KUGOMBEA UBUNGE


MSANII wa bongo ‘muvi’, Baby Mahada, amesema kuwa malengo yake aliyojiwekea ni kuja kugombea ubunge  kwa kuwa anaamini ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, msanii huyo alisema kuwa hashindwi kuwatumikia wananchi hivyo baada ya miaka kadhaa atakuwa katika mchakato huo.

Alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya kutaka kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na vitendo vya baadhi wanasiasa kutowajali wananchi ambao ndiyo waliyowapa dhamana za kuwa katika nafasi zao.

“Malengo yangu ni kuja kuwa mbunge na kikubwa ambacho nataka kukifanya ni kuwatumikia Watanzania, ambao kila
siku wanalia juu ya wasansiasa ambao wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya maisha yao binafsi,” alisema Baby Madaha.

Hata alipoulizwa ni chama gani atakitumia katika mchakato wake huo, alijibu kuwa hataki kuweka wazi chama chake lakini muda ukifika kila mtu ataweza kujua.
“Sitaki kuweka wazi kwa sasa lakini naamini muda utakapofika kila mtu ataweza kutambua ni chama changu” aliongeza Baby.

0 comments:

Post a Comment