Monday, February 20, 2012

JON MYUZIK SASA KUJA NA FILAMU

Jon Myuzik

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Jon Myuzik, amesema anafikiria kucheza filamu lakini siyo za mapenzi kama ilivyo kwa wasanii wengine ambao wengi hawana mabadiliko katika kazi zao wanazocheza.
Jon alisema anaweza kucheza filamu lakini hatofanya kazi na nyota ambao wanamaringo kwa mafanikio yao waliyoyapata, na anaamini kazi hiyo haina mwenyewe lakini wapo wasanii wanaofanya vizuri.

“Nitafanya kazi hii ambayo hivi sasa ina idadi kubwa ya wasanii ambao wengi wao wanauza sura, bila kujua Watanzania wanahitaji nini hasa kipindi hiki ambacho kuna matatizo katika jamii zetu,” alisema Jon.

Jon alisema hata hivyo tayari ameshaanza mazungumzo na baadhi ya wasanii ambao anaamini wataweza kucheza katika filamu yake ya kwanza.

“Mazungumzo yanafanyika na baadhi ya wasanii ambao naamini nitaweza kucheza nao, lakini kabla ya yote lazima kwanza wanipe kwanza mfumo wa filamu  unavyokuwa,” Aliongeza Jon.

0 comments:

Post a Comment