Mwalimu
Vitus Lawa akikabidhi fomu ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la
Kalenga kwa Katibu wa Wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo katika
ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga mjini Iringa.
Mwalimu
Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za
kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
Mwalimu
Vitus Lawa akizungumza na wadau waliomsindikiza kurejesha fomu za
kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa chadema jimbo la Kalenga
======== ====== ========
MWALIMU AJITOKEZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Na Denis Mlowe,Iringa
MWALIMU
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngwelo iliyoko Lushoto mkoani Tanga, Vitus
Lawa (41) amejitokeza kuwania ubunge katika jimbo la Kalenga mkoani
Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akitumia
msemo wa neno ‘Jembe ambao kila herufi imebeba maana ya ujumbe, Lawa
aliyesindikizwa na baadhi ya wanachama wa Chadema wa kata ya Kalenga
alilirudisha fomu za Chadema kwa kuwapa moyo wakazi wa Kalenga kuwa
mkombozi wa kweli amefika katika kuwaletea maendeleo.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya kurudishafomu mbele ya Katibu wa Chadema
wilaya ya Iringa Vijijini Felix Nyondo, Lawa alisema uwezo wa kuwakomboa
na kuwaletea maendeleo wakazi wa Kalenga umefika hivyo ni wakati wake
wa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo katika kushirikiana na kushikamana
katika kuleta maendeleo.
Alisema
endapo atapatiwa nafasi atatumia ajenda tano ambazo zinamaana ya neno
jembe, imebeba maana kubwa sana katika maisha ya binadamu kwa uwezo
wangu wa akili na ubunifu,neno hilo lina maana ya jamii bora ambayo
itatokana na kuwajengea uwezo kwa wajasiliamali wote na elimu bora pia
inawezekana kwa wakazi wa Kalenga kwa kusimamia upatikanaji elimu
iliyobora kwa taasisi husika na wadau wake.
Lawa
alisema endapo chama kitampitisha kuwania ubunge kwa jimbo la Kalenga
atawaletea maendeleo wakazi hao kwa kuhakikisha miundo mbinu inakuwa
bora kwa wilaya hiyo kwa kuanzisha shirika la wakandarasi ambao
watasimamia kitengo hicho.
Aliongeza
kuwa kuwainua wafanyabiashara wa jimbo la Kalenga kupitia mafunzo ya
ujasiliamali na kuanzisha shirika la wafanyabiashara wa kalenga walioko
nje na ndani ya mkoa wa Iringa.
“Nitaakikisha
naanzisha kundi la wana Kalenga waishio ndani na nje ya mkoa kushiriki
kikamilifu katika kuleta maendeleo ya jimbo kwa mtindo wa egima hivyo
najiamini nina uwezo wa kuwasaidia wananchi wa Kalenga na siasa safi kwa
wananchi ni JEMBE” alisema Lawa
Hadi
sasa kuna wanachama 13 wa Chadema wamejitokeza katika ofisi za chama
hicho wilaya ya Iringa vijijini kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya
kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Kalenga katika Uchaguzi
mdogo wa kujaza kiti hicho kilichoachwa wazi na Dk William Mgimwa
aliyefariki Januari 1, mwaka huu, utafanyika Machi 16, mwaka huu.
Wananachama
wengine waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hiyo kuwa ni pamoja na
Lawa ni Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega,
Rehema Makoga, Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, Mussa
Mdede, Mchungaji Samweli Nyakunga, Daniel Luvanga na Anicent Sambala.
0 comments:
Post a Comment