Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media,
Yusuf Bakhresa akisalimiana na wasanii wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.
Baadhi ya wasanii
maarufu nchini wakiwa na Meneja wa Uhusiano wa AzamTV, Maryam El-haj
wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WASANII wa filamu nchini, wamekiri kufurahishwa kwao na ujio wa kituo cha Teevisheni cha Azam (Azam Tv) na kuutaja kama ukombozi utakaochagiza maendeleo ya sanaa na wasanii ndani na nje ya nchi.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao Makuu ya Kampuni ya Azam Media
Ltd, wasanii hao, Jacob Steven ‘JB’, Mahsen Awadh ‘Dk Cheni’, Yvone Cherry
‘Monalisa’ na Suzan Lewis ‘Natasha,’ walisema kama wasanii wanatarajia mengi
yaliyo bora kutoka Azam Tv.
Kwa upande wake JB alisema sanaa ya Tanzania hususani ya filamu na wadau
wake, wamepata sehemu muhimu itakayosaidia kukuza sio tu kiwango cha ubora wa
kazi zao, bali pia pato la wasanii kutokana kutokana na mikataba ya matangazo
ya muvi zao.
“Tuna matumaini makubwa kwamba ujio wa Azam Tv ni moja ya njia
zitakazoboresha kazi na pato la wasanii. Ni fursa nyingine ambayo wasanii
tunapaswa kuitumia vema ili kuwafikia wadau wetu kupitia,” alisema JB mmoja wa
wasanii nguli wa Bongo Muvi.
Monalisa, yeye alibanisha kuwa matarajio ya wasanii wengi ni kuwa ujio huo
wa Azam Tv utakwenda sambamba la ongezeko la mikataba ya kurushwa kwa filamu
zao, kwani kabla ya hapo kulikuwa na mikataba michache.
“Naamini hii ni moja ya neema miongoni mwa wasanii, lakini kwa sanaa na
wadau wake kwa ujumla. Tutapata mikataba minono ya kurushwa kwa filamu zetu
hapa na kutanua pato letu. Hakika nimefurahia ujio wa Azam Tv,” alisema
Monalisa.
Dk Cheni naye hakuwa mbali na maoni ya wenzake, akisema anaamini fursa ya
wasanii kuwafikia wadau na wadau kupata vilivyo bora kutoka kwao imepata
kiunganishi muhimu ambacho ni Azam Tv.
“Kwangu mimi Azam Tv ni zaidi ya kituo cha Televisheni. Nakichukulia hiki
kama kiunganishi muhimu cha sisi kuwafikia mashabiki wetu, lakini wao pia
kutuona kwa mapana na kuchangia maendeleo ya sanaa na wasanii Tanzania,”
alisema Dk Cheni.
Natasha yeye kwa upande wake aliupongeza uongozi wa Azam Media kwa kuwajali
wasanii kwa kuanzisha chaneli ya Sinema Zetu inayopatikana katika king’amuzi
cha Azam Tv na kwamba anaamini itakuwa chachu kuu ya mafanikio ya sanaa
nchini.








0 comments:
Post a Comment