
Mshehereshaji Bw. Salum Msellem
kutoka Istiqama Radio akitambulisha meza kuu kwa washiriki wa mafunzo ya
Ujasiriamali ya siku moja kwa Vijana Visiwani Pemba yaliyofanyika
mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Madungu.

Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw.
Mohammed Ali, akisoma taarifa ya maendeleo ya vilabu vya Umoja wa
Mataifa visiwani humo na changamoto zinazowakabili kwa walezi wa vilabu
hivyo.
.Vijana waaswa kujikita katika ujasirimali ili kuondokana na umaskini
Na Mwandishi Wetu
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC), kilifanya mafunzo yenye tija ya ujasirimali kwa vijana katika
Mji wa Pemba visiwani, Zanzibar na kupata washiriki wenye kiu ya kutaka
kujiajiri na kuondokana na umasikini hapa nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa
mafunzo hayo ya siku moja ya ujasirimali kwa vijana hivi karibuni Mjini
Pemba, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC),
Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2000
walizindua malengo ya milenia ili kusaidia nchi zinazoendelea kuondokana
na umaskini.
“malengo manane ya milenia ni pamoja
na Afya ya Uzazi kwa kinamama, Elimu, kuondoa umaskini na mambo ya
mazingira vile vile kusaidia mikakati mbalimbali ya nchi hizo katika
utekelezaji wake mpaka kufikia mwaka 2015,” amesema Bi. Ledama.

Afisa Vijana - Mshauri kutoka WIZARA
ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Bi. Stara
Salim akizungumzia jitihadi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika
kuwawezesha Vijana kupata mikopo kupitia asasi mbalimbali za fedha ili
waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na lindi la umaskini visiwani
Pemba.
Amesema kwamba kazi kuu ya Umoja wa
Mataifa na taasisi zake ni kusaidia Serikali mbalimbali katika nchi
zinazoendelea kufanikisha mikakati na utekelezeji wa malengo ya milenia
ikiwemo dhana ya kupunguza umaskini.
Bi.Ledama alilisitiza kwamba katika
utekelezaji huo Umoja wa Mataifa inasaidia mikakati hiyo ya kuondoa
umaskini kwa kuandaa program mablimbali na kufanya mafunzo ya
ujasirimali kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuondokana na umasikini.
“Serikali pekee haiwezi kutoa ajira
kwa watu wote kwa sababu nafasi ni chache na mahitaji ni makubwa kwa
hiyo ndugu zangu kujiajiri na kuajiri wengine katika sekta binafsi
kupitia ujasirimali ni nafasi pekee ya kuondokana na umaskini,”
aliongeza.
Amesema kwamba asilimia 43 ya wakaazi
wa Zanzibar ni vijana kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa kwa Umoja wa Mataifa
na sekta binafsi kuhamasisha ujasirimali kama njia pekee ya kujiajiri
na kuondokana na umaskini wa kipato na wa jumla.

Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumzia lengo la
kuendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu walio nje ya shule ikiwa ni
moja ya agenda ya kutekeleza malengo ya milenia ya kupunguza umaskini
kwa nchi zinazoendelea.
Bi. Ledama amesema sekta binafsi kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaweza kupunguza tatizo la ajira
kwa kusisitiza ujasirimali zaidi katika maeneo mbalimbali ya Bara na
Visiwani.
“Haya ni mafunzo ya pili kufanyika
bara na visiwani yenye kutoa mafunzo yenye tija juu ya ujasirimali na
faida zake katika kupunguza na kupambana umasikini kwenye nchi
zinazoendelea,” aliongeza.
Amesema kwamba Shirika la Kazi
Duniani (ILO) wana kitengo maalum cha mambo kujenga uwezo kwa vijana na
mafunzo ya ujasirimali yenye lengo la kuondoa umasikini miongoni mwa
vijana nchini Tanzania.

Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali
kupitia Program ya kazi Nje nje inayolenga kuelemisha Vijana stadi za
Ujasiriamali iliyoasisiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bi. Mwanapili
Hamad akitoa mada kuhusu dhana nzima ya uongozi katika biashara
(Business Management) kwa wajasiriamali Vijana visiwani Pemba ili waweze
kuboresha kipato chao.

Picha juu na chini ni sehemu ya
washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja yaliyoratibiwa na
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).


Mjasiriamali mwenye kipaji cha
kuchora ramani za majengo, kutengeneza sampuli za nyumba kwa kutumia
maboksi Bw.Steven Timothy Mihale kutoka Temeke Youth Development Network
(TEYODEN) akionyesha moja ya kazi zake kwa wajasiriamali wenzake
ambayo inampatia kipato na kuweza kuendesha maisha yake.
Bw. Steven Mihale aliwapa moyo wajasiriamali wenzake na kuwataka kuwa na uthubutu na kutokata tamaa mapema.

Vijana wajasiriamali wakiangalia kazi ya Mjasiriali mwenzao.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo
akiuliza swali kwa wakufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoratibiwa
na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali
Bi. Mgeni Salum akitoa somo la namna ya kuhifadhi hesabu za mauzo na
kujua kama biashara ina faida au hasara sanjari na kupata mikopo kupitia
taasisi za kifedha.

Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw.
Mohammed Ali akiteta jambo Mkutubi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha (katikati) wakati wa mafunzo ya
Ujasiriamali kwa vijana visiwani Pemba yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
shule ya Sekondari Madungu.

Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akifunga mafunzo ya
siku moja ya wajasiriamali Visiwani Pemba yaliyoratibiwa na kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).








0 comments:
Post a Comment