
TAMKO
LA WENYEVITI WA CCM-MIKOA LA KUMPONGEZA KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABRAHAMANI
KINANA NA SEKRETARIETI YA CCM TAIFA.
LEO TAREHE 10/DESEMBA/2013
OFISI NDOGO YA CCM DAR- ES- SALAAM
Sisi Wenyeviti wa CCM-Mikoa tuliokutana
leo Tarehe 10/Desemba/2013 hapa Dar es salaam, kwa kauli moja na kwa niaba ya
wanaCCM wa mikoa yetu, tunatoa kauli ya kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi ndugu Abrahamani Kinana na Sekretarieti yote kwa utekelezaji
uliotukuka wa majukumu yao ya kichama. Tangu alipopewa wadhifa wa Ukatibu Mkuu
ameonyesha uwajibikaji mkubwa, uliokiwezesha Chama kupata uhai mpya na kuamsha
Ari na matumaini zaidi ya Watanzania kwa Chama Cha Mapinduzi.
WanaCCM nchini tuko katika mstari wa
mbele kuisimamia Serikali yetu kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015
sura ya Tisa; Inayokitaka Chama kuisimamia Serikali yake.
Kwa pamoja tunaungana na kupinga kwa
nguvu zote mambo yafuatayo;
1. Ubadhirifu
unaofanywa katika Serikali za Mitaa nchini unaozifanya Halmashauri nyingi kujirudiarudia
kupata hati chafu na zenye mashaka, inayosababisha hasara na manung’uniko kwa
wananchi.
2. Utelezaji
duni wa baadhi ya miradi ya maendeleo unaopelekea kuwepo kwa huduma duni na
zisizokidhi thamani ya fedha na matakwa ya kitaalamu. Hii inaashiria uwepo wa
Rushwa na ubadhirifu wa fedha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.
3. Ucheleweshaji
wa maslahi na stahiki za watumishi wa Umma kunakopelekea kuwa wavunja moyo na
ari watumishi, katika kutekeleza majukumu yao na hivyo kusababisha kutokea kwa
migomo ya mara kwa mara kufuatia uzembe katika kuwapatia haki zao, kinyume na
misingi ya utawala bora.
4. Gharama
kubwa ya uendeshaji wa shughuli za Serikali na Taasisi zake ikilinganishwa na
gharama zinazotumika kwenye miradi ya maendeleo na uboreshwaji wa huduma za
jamii kwa wananchi.
5. Usimamizi
mbovu wa Operation mbali mbali za Serikali zenye nia njema kwa Taifa. Mfano
Operasheni kuhamisha wafugaji na Operasheni Tokomeza; Zina nia njema lakini
usimamizi wake umekuwa mbovu hata kupelekea kuvuruga nia yake njema kwa Taifa.
6. Kushindwa
na Kuchelewa kutatua baadhi ya Kero sugu kwa Wananchi kama malalmiko mbali
mbali ya wakulima (mfano mbolea za minjingu kutofanya vizuri kwa asilimia
kubwa, matatizo ya wakulima wa pamba na korosho nk.) na wafugaji; Rushwa
zilizokithiri katika sehemu mbali mbali za utoaji wa huduma kwa wananchi na
ucheleweshwaji wa fadha za miradi ya maendeleo nk.
Katibu Mkuu wa
CCM daima amekuwa akikemea kwa nguvu zote madhaifu yote tuliyoyataja hapo juu
na sisi kama Wenyeviti wa CCM Mikoa yote Tanzania. Tunaitaka Serikali ichukue hatua za haraka katika kurekebisha madhaifu
hayo. Viongozi na watendaji wengine wote wa Serikali, walioonesha udhaifu
mkubwa katika kutekeleza majukumu yao, na ambao walipewa wito na wengine ambao
wanatakiwa kupewa wito; wa kuhudhuria mbele ya Kamati Kuu ya CCM wachukuliwe
hatua zinazostahili. Tunawakumbusha viongozi wa Serikali watambue kuwa Chama
cha Mapinduzi kinaisimamia Serikali kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 Sura ya Tisa.
_______________________________________________
Mgana Izumbe Msindai – Mwenyekiti wa
Wenyeviti Mikoa
______________________________________________________
Haji Juma Haji – Makamu Mwenyekiti Wa Wenyeviti Mikoa
______________________________________________
Lucas Ole Mukusi – Katibu wa Wenyeviti
Mikoa
TUNAWASILISHA








0 comments:
Post a Comment