
Dar
es salaam, Tanzania
Sheria
za kulinda haki za mteja zinampa uwezo mtu yeyote haki ya kudai fidia juu ya bidhaa
ambao haiendani na thamani ya kiasi alichotoa au bidhaa ambayo haina kiwango. Sheria
hizi zimetungwa ili kuwakabili wauzaji wa bidhaa na watoa huduma kuwajibika
katika biashara zao moja kwa moja pale wanapofanya biashara kinyume na sheria
zilizopo.
Katika
harakati za kulinda wateja wake, kampuni ya Samsung imezindua mfumo maalum wa kuangalia
uhalisia wa bidhaa zake zinunuliwazo unaojulikana kama ‘e-warranty’
unaomuwezesha mteja kugundua simu halisi za Samsung kwa kupitia namba maalum za
kimataifa za kujua mahala simu imesajiliwa yaani namba za IMEI. Huduma hii ya
dhamana ya ziada inatoa ofa kwa wateja wote wa Samsung nafasi ya kipekee ya
kuangalia uhalisia wa bihdaa.
Moja
kati ya changamoto kubwa katika soko la simu nchini Tanzania leo hii ni kwamba
soko limegubikwa na bidhaa feki, mbovu na zisizo na dhamana. Ni vigumu kwa mteja
kujua ipi bidhaa halisi na ipi sio. Samsung inaamini kwamba mteja anatakiwa awe
na huduma ambayo itampa fursa ya kuangalia uhalisia wa simu yoyote atakayonunua
na ndio maana wao wamekuja na huduma hii muhimu katika kulinda haki ya mteja.
Huduma
hii ya dhamana inafanya kazi katika nchi 15 tu za Africa ambapo ili mteja aweze
kupata huduma hii itakayompa dhamana ya miaka miwili atatakiwa kujisajili kwa
kutuma tarakimu 15 zilizo nyuma ya simu hiyo. Nchi nyengine yenye huduma kama
hii ni Afrika ya Kusini, Nigeriia, Kenya, Ghana, Sudan, Ethiopia, Namibia,
Zambia, Mauritius, Uganda, Ivory Coast, Angola, Botswana, and Msumbiji.
Katika
kuhakikihsa elimu ya huduma hii muhimu kwa Watanzania inasamabaa kwa haraka
zaidi, Samsung Tanzania ilizindua promosheni kabambe katika msimu huu wa
sikukuu za mwisho wa mwaka inayojulikana kama Pambika na Samsung itakayodumu mpaka Desemba 23, 2013. Promosheni
hiyo inalenga kuhamasisha wateja kununua bidhaa halisi na kuzisajili kasha
kuzawadiwa katika droo za kila wiki na droo kubwa ya mwisho wa promosheni.
Akizungumza
wakati wa droo ya nne ya kila wiki ya Pambika na Samsung, Bw. Sylvester Manyara
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania amesema kwamba Samsung
inadhamira ya dhati katika kulinda haki za mteja na kumlinda kutokana na bidhaa
feki ambazo zipo kila kona kwa sasa. “Wateja wote wana haki ya kujua kuhusu
umiliikaji wa bidhaa zao wakati wa kununua. Ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa
Samsung tunajitolea kulinda haki za wateja kwa kuwapa wateja wetu jukwaa la kufurahia
uamuzi wao wa kununua bidhaa halisi” alisema Bw. Manyara.
Droo
ya nne imetoa washindi 15 wengine ambao wamepokea bidhaa mbalimbali toka
Samsung kama Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 toka Samsung, Luninga ya LED 32’,
Kompyuta mpakato, Jiko la kupashia chakula, Muziki wa nyumbani pamoja na deki
za DVD toka Samsung. Jumla ya wateja 60 kutoka mikoa mbalimbali tayari
wameshapatikana.
Washindi
wa wiki hii walikuwa ni…………………………….
Hii
ni aina nyengine ya huduma iliyoletwa na Samsung ili kulinda haki za wateja na
kuwalinda kutokana na madhara ya kununua bidhaa feki. Pambika na Samsung
inawazawadia wale wote wanaonunua na kusajili bidhaa halisi za Samsung kila
wiki kabla ya kutolewa kwa zawadi kubwa ya gari jipya la Mitsubishi Double
Cabin itakayokuwa imesheheni bidhaa zote zinazotoka kila wiki ambapo mteja
mmoja mwenye bahati atajinyakulia hapo Desemba 23, 2013.








0 comments:
Post a Comment