Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC wa
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro wakiteremka kwenye
Treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Stesheni ya
Mlimba, mkoani Morogoro jana, tayari kwenda kuwasalimia wafuasi wa CCM
pamoja na wananchi wakiwa safarini kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda
Dar es Salaam. Kinana na msafara wake walikuwa katika ziara ya siku 26
katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njomba kuimarisha uhai wa chama
na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata
Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Kinana na Nape wakimwangalia Dk. Migiro akiteremka kwenye treni hiyo katika Stesheni ya Mlimba.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwa na Katibu wa CCM
Kata ya Mlimba Selemani Balali wakati msafara wa Kinana ulipoteremka
kwa muda katika Stesheni ya Mlimba.
Nape akiangalia samaki waliokuwa wakiuzwa katika stesheni la Mlimba, Kulia ni Dk. Migiro.
Kinana, Migiro na Nape wakiwa na baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Mlimba alipotembelea Stesheni ya Mlimba.
Komredi Kinana akiwa na Katibu wa CCM,Kata ya Mlimba Selemani Balali
alipokuwa akielekea kupanda treni katika Stesheni ya Mlimba, Morogoro
kwenda Dar.
Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi katika Stesheni ya Mlimba
Jopo la wanahabari wa Televisheni, magazeti, Redio na mitandao ya
Kijamii (Bloggers), walioambatana na msafara wa Komredi Kinana wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kuwasili salama katika Stesheni ya Dar
es Salaam leo asubuhi.
Kinana akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida baada ya kuwasili salama katika Stesheni ya Dar es Salaam leo
asubuhi.
Dk. Migiro akilakiwa na Madabida
Nape akikukbatiwa kwa furaha na madabida ya kuwasili Dar es Salaam leo.
Kinana akivalishwa skafu na Chipukizi alipowasili Dar es Salaam leo.
Komredi Kinana, Nape Nnauye na Dk. Migiro wakiwasalimia wafuasi wa CCM
waliofika kuwalaki katika Stesheni ya Tazara, Dar es Salaam.
Komredi Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM
Dk. Migiro na Nape wakiimbiwa wimbo
Madabida akihutubia wakati wa mapokezi hayo
Nape akiwashukuru wanahabari waliombatana nao kwenye msafara katika ziara ya siku 26 katika mikoa minne.
Kinana akihutubia na kutoa shkurani kwa mapokezi hayo pamoja na
wanahabari alioambatana nao kwenye ziara hiyo, akiwemo mmiliki wa Blogu
hii ya Kamanda wa Matukio, ambaye pia ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la
Jambo Leo, Richard Mwaikenda.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu (wa pili kulia) akiwa miongoni mwa wanaCCM waliofika kuulaki
msafara wa Kinana.
Kinana akiwashukuru wanahabari alioambatana nao kwenye ziara hiyo.
Kinana akimkumbatia mtangazaji wa Redio Uhuru, Sheila Simba
Nape akikukmbatiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe
Kinana akimkumbatia mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Star, Joseph
Mpangala. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA Blog ya Kamanda wa
Matukio.
0 comments:
Post a Comment