
Ile
ishu ingekuwa kuleeee Bongoland……Kwanza kungeundwa Kamati ya mazishi ambayo ingepewa uwezo wa
kutoa mikataba ya shughuli mbalimbali ambazo zingetakiwa kufanyika.
Kwanza
ingetolewa tenda ya kukarabati uwanja wa ndege wa kijiji kwenye mazishi,
tenda ya kukarabati mabarabara ya kuelekea kijijini huko, pia kungetakiwa kuagiza
ambulensi bullet proof kwa ajili ya kusafirisa mwili toka hospitali mpaka
eapot, pia ingetolewa tenda ya kuagiza magari 20 ya kifahari ya kusindikiza mwili.
Jamaa zetu wangepewa
tenda ya kujenga jukwaa na kuratibu shughuli zote za kuaga mwili pale Leaders
Club.
Burudani
zingesimama kwa miezi mitatu, kiukweli hapa wanamuziki wangekatazwa kupiga
muziki miezi mitatu lakini redio na TV zingepiga tu kama kawaida, na sanaa
nyingine zingeendelea tu.
Yunifom
za wahudumu wa shughuli
zingeagizwa toka Uholanzi japo kuwa zimetengenezwa Uchina. Wananchi
wangehamasishwa kuvaa yunifom hizi kuonyesha uzalendo, zingeuzwa kwa bei
rahisi, Tshirt 20,000/- tu.
Mashirika
yangeshindana kutoa rambirambi kwenye magazeti, TV na radio, matangazo
haya yangefanyiwa tathmini ya undani gharama zingefikia
mabilioni kadhaa.
Wanamuziki wangepishana studio na kutoa singo ambazo
zingeuzwa na wasio wanamuziki na kuingizia watu mkwanja wa ukweli na
kuwaacha
wanamuziki wanadaiwa malipo ya studio.
Mablog yetu yangejaa vichwa vya
habari..Ona picha za mwisho za marehemu akiwa mochwari, Ingia hapa uone
chumba
alicholala marehemu alipotembelea Iringa, Pata picha ya nyumba ndogo wa
marehemu akilia, ingia hapa uone picha za nyumba ndogo ya rafiki yake
mdogo wake marehemu akiwa kavaa kanga moja akielekea bafuni na
kadhalika. Baada ya hapo Wabunge wangekuja juu kuhusu matumizi
makubwa ya shughuli hiyo na kuomba tume iundwe kuchunguza matumizi ya Kamati ya Mazishi, kwa kuwa uchaguzi uko mbali ishu ingekufa
baada ya siku chache kama ile ishu ya matumizi ya miaka 50 ya nanihii.








0 comments:
Post a Comment