
Wanafunzi
wa shule za sekondari kote nchini wameaswa kutumia vizuri maendeleo ya
teknolojia yanayotokea kwa sasa ili kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.
Madai
hayo yalitolewa na Meneja Biashara wa Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel kanda ya ziwa Raphael Daudi wakati akikabidhi kompyuta kwa
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kalangalala iliyopo mkoani Geita.
Meneja
huyo alisema kumekuwa na wimbi la wanafunzi ambao hutumia kompyuta kwa
matumizi ambayo ni kinyume na maadili na kusababisha jamii kuelekea
kwenye mkondo tofauti na uliokusudiwa.
“Baadhi
ya wanafunzi wamekuwa wakibatilisha matumizi ya kompyuta kwa kujifunza
mambo yasiyofaa badala ya kuitumia kupanua uelewa wao wa masomo.
Wanasahau kuwa kufanya hivyo maadili humomonyoka kwa kiasi kikubwa
katika jamii yetu,” alisema Daudi.
Kwa
upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kalangala, Deusdedith
Omchamba alisema mpango wa kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu kwa
kusababisha matokeo makubwa kwa wanafunzi unaofahamika kama “Big results
now” utafanikiwa katika shule hiyo kwa kutumia teknolojia ya kompyuta
kujifunzia.
“Teknolojia
ya kompyuta ni muhimu sana kwa maendeleo ya wanafunzi kwa sasa kwani
wanafunzi wanaweza kutumia kompyuta kusomea na hata kutafuta habari
mbalimbali zinazoshabihiana na masomo yao,” alisisitiza Mwalimu
Omchamba.
Aliongeza
kwa kusema kuwa ni jukumu la wanafunzi kutambua umuhimu wa teknolojia
hiyo na kuitumia vyema kwa kujiendeleza katika suala la elimu zaidi
kuliko mambo mengine ambayo hayana kipaumbele kwa jamii yetu ya
Tanzania.
Baadhi
ya wanafunzi katika shule hiyo walielezea hisia zao na kusema kuwa
wanafurahia sana kuwa na somo la kompyuta shuleni hapo na pia
watajitahidi kutilia maanani ushauri uliotolewa na Meneja biashara wa
Airtel kuhusu matumizi yanayofaa.
Pamoja
na kutoa vitabu kwa shule za sekondari nchini Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel Tanzania imekuwa ikisaidiana na serikali kuhakikisha
kiwango cha elimu kinaimarika na kuleta mapinduzi katikla sekta hiyo
kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.








0 comments:
Post a Comment