
WAKALA
wa Umeme Vijijini ( REA) unatarajia kutekeleza awamu ya pili ya kusambaza
nishati hiyo kwenye wilaya sita za mkoa
wa Morogoro kwa gharama ya Sh bilioni 21.5
katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Miradi
hiyo iliyo kwenye mchakato wa kupata wakandarasi imepangwa kuanza kukelezwa
mwezi ujao. Vijiji zaidi ya 30 vilivyo katika
Wilaya
za
Gairo, Kilombero, Ulanga, Mvomero, Kilosa na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro
vitanufaika.
Meneja
wa Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Morogoro, Deogratias Ndamugoba, alisema
hayo juzi kwenye taarifa yake kwa Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri
Muhongo alikwenda kuzindua mradi wa Rea katika Kijiji cha Berega kilichopo
wilayani Kilosa.
Alisema
miradi ya umeme ya Rea awamu ya kwanza, katika mkoa wa Morogoro inatekelezwa
wilaya ya Kilosa, Ulanga na Kilombero.
Vijiji
vya wilaya ya Kilosa vilivyonufaika katika awamu ya kwanza na wilaya kwenye
mabano ni Kwambe, Maguha, Magumbike, Kiyengea, Gongoni, Mgugu, Berega,
Mbegesela, Kisanga, Tazama, Kisanga, Kidodoo, Msolwa Sekondari na Msolwa.
Wilayani
Ulanga vijiji vinavyonufaika ni pamoja na Mzelezi, Chilombola, Mwaya, Ruaha,
Ngoheranga, Kiswago, Tanga, Mwembeni, Malinyi, Sofi, Manda Juu, Mtimbira,
Kipenyo na Itete.
Kwa
upande wa wilaya ya Kilombero, vijiji vilivyonufaika ni Mpanga Misheni, Utengule, Ngalimila na Kisawasawa. Miradi
yote imegharimu Sh bilioni 14.8.
Wakati
huo huo, wananchi wa vijiji vilivyopitiwa na miradi hiyo ya Rea
wameipongeza serikali ya awamu ya nne kuwapunguzia gharama ya
kuunganisha umeme katika makazi yao.
Wananchi
hao walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti mbele ya Waziri Muhongo, ambaye
alifanya ziara kwenye vijiji vilivyo kwenye mpango wa awamu ya kwanza ya
kupatiwa umeme wa Rea.
Wakazi
wa Kijiji cha Mtombozi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema serikali imewapa faraja kutokana na
kuwaunganishia umeme.
“Serikali
imetupa faraja sisi wananchi wa vijijini, kwani tunatambua umuhimu wa umeme
katika kutuletea maendeleo yetu ya kiuchumi na kuboresha huduma za kijamii kama
afya na elimu,” alisema
Zainabu Salum.
Kwa
upande wake, Paroko wa Parokia ya
Bunduki, Padri Godfrey Lembele akizungumza mbele ya Waziri Muhongo, alisema
kufikishwa umeme katika kijiji cha Bunduki, tarafa ya Mgeta kutawezesha wananchi kukuza kipato.
Alisema
hayo ni mapinduzi makubwa ya kuondokana na umaskini kupitia nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Beraga inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya
Morogoro, Mchungaji Isaac Mgego, alisema
wamepunguziwa gharama ya matumizi ya
mafuta
ya
kuendeshea jenereta ambapo kwa mwezi
walikuwa wakitumia Sh milioni
moja.
“Tunaishukuru
Serikali, imetimiza ahadi yake iliyotolewa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa,” alisema Mchungaji Mgego.
Hospitali ya Berega ilianzishwa na wamisionari
wa kanisa hilo mwaka 1879 ambapo umeme umeingizwa miezi mitatu iliyopita.
Katika
mikutano yake ya hadhara kwenye vijiji alivyotembelea, Waziri aliwaambia
wananchi serikali imepunguza gharama za
kuingiza umeme vijijini na kuwa Sh 177,000.
Alishauri
wananchi kutumia fursa hiyo kwa kulipa kwa awamu wanufaike na umeme
utakaokuza uchumi wao kupia ya kilimo, biashara na uanzishwaji wa
viwanda vidogo vidogo vijijini.








0 comments:
Post a Comment