2:17 AM
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika
wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako
ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya. Pichani, Kinana na wajumbe wa
sekretarieri ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose
Migiro (Siasa na Uhusiano wa KIImataifa), wakiwapungia mikono wananchi
wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea katika bandari ndogo ya Mbamba Bay,
kuanza safari ya kwenda Kyenla. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa,
Ernest Kahindi
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Mbamba Bay, Nyasa, kabla ya kupanda meli kwenda Kyela
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migirob akisalimiana na Nahodha wa Mv Songea
Tom Faya, katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani
Ruvuma kabla ya safari ya kwenada Kyela
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akisalimiana na Nahodha wa mv Songea, kabla ya safari ya kwenda Kyela
kutoka bandari ndogo ya Mbamba Bay, Nyasa. Wapili kulia ni Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa
Oddo Mwisho
Mkurugenzi na Mtayarishaji Mkuu wa
theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ni baadhi ya abiria walioko
katika msafara wa Kinana,akipanda mv Songea.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akipanda mv Songea. Wanaomfuata na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo
Mwisho na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro.
Wananchi na wanachama wa CCM wa Mbamba
Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, wakisindikiza kwa boti mv Songea
wakati ikiondoka bandarini
Nahodha wa ,mv Songea na Kinana wakizungumza na waandishi wa habari. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
0 comments:
Post a Comment