| Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu kushoto akipokea tuzo ya heshima ya sheria za vita kutoka kwa mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria Jane Massey huku wanafunzi walioshinda wakishuhudia zoezi hilo leo |
| Washindi wa tuzo hiyo chuo kikuu cha Iringa wakiwa na tuzo yao kushoto ni mkuu wa chuo Prof Nicholaus Bangu na kulia wa kwanza na mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria Bi Jane Massey |
| Mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha Iringa Jane Massey akikabidhiwa tuzo ya heshima ambayo chuo hicho kimeshinda katika mashindano yaliyoshirikisha nchi saba Afrika na chuo hicho kunyakua tuzo hiyo kwa kuwa chuo cha kwanza |
| Mkuu wa chuo cha Tumaini ( chuo kikuu cha Iringa ) Prof Nicholaus Bangu akionyesha tuzo ya heshima ya sheria za kivita ambayo chuo chake kimeiwezesha Tanzania kufanya vema |
| Washindi wa tuzo hiyo wakiwa na vyeti vyao katika picha ya pamoja na mwalimu Dr Chachage
………………………………………………………………………..NA FRANCIS GODWIN BLOGU,IRINGA
Tanzania
yazibagwa nchi sita barani Afrika katika mashindano ya vyuo vikuu ya
kuwania tuzo ya heshima ya sheria za vita yaliyomalizika hivi
karibuni .
Katika shindano hilo lililofanyika kati ya Novemba 16-23 mwaka huu jijini Arusha chuo kikuu cha Iringa kiliwakilishwa na washiriki watatu ambao ni Anneny Nahum ,Janeth Nagai na Joanna Mcintype vijana hao waliweza kufanya vema kiasi cha kuiwezesha nchi ya Tanzania kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo. Wakizungumza leo chuoni hapo katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa uongozi wa chuo hicho ,washirikia hao walisema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano ulioonyeshwa na nidham iliyotukuka miongoni mwao. Hata hivyo walisema kuwa tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania na ni heshima kwa chuo hicho . mkuu msaidizi wa kitivo cha sheria chuo kikuu cha Iringa Jane Massey alisema kuwa washiriki hao wamepata kushinda kutokana na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika mashindano hayo na kuwa heshima kubwa ambayo chuo hicho imepata ni jambo na kujivunia na kumshukuru Mungu pia. Alisema kinachoangaliwa katika mashindano hayo na lengo la tuzo hiyo ni kuenzi amani na kuona hakuna matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yanatokea wakati wa vita ,hivyo sheria hiyo inapaswa kuendelea kutolewa hata kwa Tanzania pia Kwa upande wake makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu alisema kuwa chuo hicho kitaendelea kufanya vema si katika mashindano pekee bali katika mambo mbali mbali yakiwemo ya kitaalum . Kwani alisema kuwa moja kati ya mambo yanayozingatiwa katika ufundishaji chuoni hapo ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi katika maadili na nidham na ndio mafanikio ya wanafunzi kufanya vema. Tuzo hiyo ambayo inatolewa kama njia ya kumuenzi aliyekuwa mwanzilishi wa msalaba mwekundi ilianzishwa mwaka 2010 na kuanza kushindaniwa mwaka 2011 ambapo ilichukuliwa na nchi ya Ephiopia ilinyakuwa kwa mara ya kwanza na mwaka 2012 ilichukuliwa na Kenya na mwaka huu Tanzania i meweza kuzishinda nchi hizo sita ambazo ni South Afrika, Uganda,Kenya, Rwanda, Ethiopia na Zimbabwe |








0 comments:
Post a Comment