* Ni kwa kuchapisha Habari, Makala za Uchochezi
* Yadai yalikuwa na lengo la kuvuruga amani nchini
SERIKALI imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kuandika habari na makala za uchochezi. Gazeti la Mwananchi linalomilikiwa na Kampuni ya Mwananchi Communications limefungiwa kwa muda wa siku 14, wakati Mtanzania linalomilikiwa na Kampuni ya New Habari 2006, likifungiwa kwa miezi mitatu, kutokana na kutaka kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
Akitoa tamko hilo la serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema kuwa serikali imefikia hatua ya kuyafungia magazeti hayo kutokana na habari za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani na vyombo vya dola na kuhatarisha amani na mshikamano uliopo.
Akizungumzia kuhusu kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi, alisema gazeti hilo limefungiwa muda wa siku 14 ambapo adhabu hiyo ilitangazwa kwa tangazo la serikali namba 333 la Septemba 27, mwaka huu.
Alisema gazeti hilo hivi karibuni lilichapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, ambapo alitolea mfano gazeti la Julai 17, mwaka huu toleo namba 4774 ilichapisha habari iliyokuwa ikisema.... Read More

0 comments:
Post a Comment