Mwanamume mmoja katika kitongoji cha
Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa ni mwanamuziki maarufu duniani ,
Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa
wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Robert Hunter, mwenye umri wa miaka
35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana
mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu.
Polisi walimkamata nyumbani kwake
akiwa na kanda 800 za video kutoka kote duniani , baadhi kutoka kwa wasichana
na nyengine kutoka kwa wavulana
Hunter alikubali mashtaka yote 15
yakiwemo kuwachochea watoto kujihusisha na vitendo vya ngono na kutengeza kanda
za video zenye picha chafu.

Mahakama ilifahamishwa kuwa kwa
miaka mingi Hunter aliwalenga mamia ya wasichana kutoka Uingereza, Ufaransa ,
Spain, Italy, Serbia, Bara Asia na Canada.
Wasichana walioamini kuwa mwanamume
huyo alikuwa kweli Justin Bieber, walijipiga picha wakiwa uchi baada ya Hunter
kuwaahidi kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao.
Hunter alijidai kuwa Justin Bieber
ili watoto wamtumie kanda za video za ngono
Kwa mujibu wa kiongozi wa mashtaka
Richard Bennet, vijana wa shule pia walinaswa katika mtego wa Hunter aliyejidai
kuwa msichana na kuwataka wafanye vivyo hivyo ambapo alitumia kanda zao
kuwatega wasichana wengine.
Lakini walipojaribu kujiondoa kwa
mtego wake aliwatumia vitisho.
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka
12, alijikata mikono yake baada ya Hunter kuchapisha picha zake kwenye mtandao
akiwa uchi pamoja na anwani yake na nambari zake za simu.
Jaji alisema hii ni kesi mbaya
kuwahi kuisikia kuhusu udhalilishaji wa watoto kwenye Internet.









0 comments:
Post a Comment