Mashabiki wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni
Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania
ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na
Multiple Channel O Africa Music Video Awards nominations anakuja
kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa
ataachia single yake mpya na ya kwanza kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo
iitwayo "Chereko Chereko" yenye mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya
studio za 'De Fatality Music" na producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka
huu alichukua tuzo ya mtayarishaji bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo
hii itapatikana kwenye mitandao yote na media zote kuanzia tarehe moja
October.
CPwaa ambaye amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile
anategemea kuachia single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo
amewashirikisha mafahari wengine wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya
kimataifa iitwayo "Cross-Borders Therapy" imekutanisha wakali kutoka
mashariki,magharibi na kusini mwa Afrika. CPwaa amemshirikisha "DBlack"
kutoka Ghana, DBlack ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye
ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel O.Kwa upande wa Afrika ya
kusini CPwaa amemshirikisha "Hip Hop Pantsula" a.k.a HHP kwenye nyimbo
hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.
HHP ni mmoja ya MaMC wakali kutoka bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya
MTV Base. Nyimbo hii itakuwa ya kwanza Afrika ambayo imekutanisha
wakali kutoka mashariki ,magharibi na kusini ( The first East,West and
South African Hip Hop Collaboration in History).Nyimbo hii pia
imefanyika chini ya producer Mesen Selekta pale "De Fatality Music"
Studio.
Kifuatacho baada ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko
Chereko itafanyiwa Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini
Afrika ya kusini. Kwa wale mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa
Cross Border Therapy ambao utatoka mwakani wataweza kuupata wimbo huo
kupitia iTunes,Amazon, Spotify na digital store zingine bila kusahau
mtandao wa "The Kleek" kwa wale watumiaji wa smartphones za Samsung na
Androids.
Asanteni sana na tuendelee kutoa support kwa wasanii wetu na muziki wetu.









0 comments:
Post a Comment