BASTOLA iliyotengenezwa
kienyeji imeokotwa na watoto wadogo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ifumbo
wilayani Chunya mkoani Mbeya ikiwa imetelekezwa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Diwani Athuman alisema jana kuwa bunduki hiyo inayotumia risasi za shotgun
iliokotwa Jumatano wiki hii saa 3:00 asubuhi.
Alisema watoto hao wa walikuwa
wakicheza uwanjani hapo ndipo walipoona
mfuko wa plastiki uliofungwa na baada ya
kuufungua wakakuta bastola
hiyo.
Kamanda Athuman alisema baada
ya kubaini kuwa ni bunduki waliipeleka kwa wazazi wao ambao kuchukua jukumu la
kuipelekea kwa uongozi wa Kijiji.
Wakati huo huo askari mgambo wa
Kijiji cha Bitimanyanga wilayani Chunya wamekamata risasi 114 za bundukia aina
ya SMG
zilizotupwa na mtu anayehisiwa kuwa jangili.
Kamanda Athuman alisema risasi
hizo pia zilikamatwa wiki iliyopita saa 9:00
alasiri katika Hifadhi ya Lukwati kijijini hapo na askari mgambo Daimon John
(32) akiwa na wenzake wawili walipokuwa
katika doria ndani ya hifadhi hiyo.
Alisema wakati wakiendelea na
shughuli za ulinzi walimkurupusha mtu mmoja ambaye alikimbia na kutupa
mfuko aliokuwa ameubeba na
ndani yake zilikutwa risasi hizo, nguo na redio ndogo.








0 comments:
Post a Comment