Thursday, December 13, 2012

NIKKI WA PILI KUACHIA BUM KUBAM,DESEMBA 21


Msanii wa Hip Hop kutoka A town maarufu kama Nikki wa pili,baada ya kufanya harakati za kuandaa dvd yake mpya ya Bum Kubam, ameweka wazi kwamba anatarajia rasmi kutoa kitaani siku ya tarehe 21 mwezi huu.hapo chini kuna sheria za hiyo dvd mpya ya Bum Kubam

BUM KUBAM DVD itasambazwa kwa mfumo mpya kabisa wa code namba uliopewa jina la MFUMO RAFIKI na utaanza kutumika rasmi tarehe 21/12/12

FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo na kuona idadi ya nakala zote alizouza, muda na mahali zilipouzwa.

2. Unazuia wauzaji feki kuuza kazi ya msanii.

3. Msanii atamfahamu kila mtu aliyenunua bidhaa yake na kuwasiliana nae moja kwa moja.

4. Wezi wote wa kazi ya msanii watajulikana hadharani.

5. Kazi ya msanii itapatikana kwa urahisi na kwa wakati.

6. Unapunguza vichocheo vya piracy kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa maelezo zaidi ni siku ya uzinduzi wa mfumo huu mpya tarehe 21/12/12.

0 comments:

Post a Comment