Monday, October 1, 2012

SERENGETI FIESTA 2012 @ LEADERS, DAR ES SALAAM...BHAAASS

 
Lile tamasha kubwa kuliko yyote hapa nchini, maarufu kama Serengeti fiesta ambalo limekuwa likizunguka mikoa ya Tanzania bara na kufikia takribani mikoa 11 sasa linaelekea katika kilele chake katika viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam siku tar 6 jumamosi  mwezi huu ambapo msanii wa hiphop kutoka nchini Marekani Leonard Roberts maarufu kama  Rick Ross atatumbuiza katika tamasha hilo.
Akizungumzia ujio wa msanii mkubwa kama huyo katika mahijiano maalum jijini Dar esSalaam jana, meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo amesema tamasha la Serengeti fiesta limekuwa likifanya vizuri sana katika mzunguko wake na kwamba watanzania wamekuwa wakifurahia uwepo wa tamasha hilo kutokana na mafanikio mbalimbambali ambayo wamekuwa wakipata kila ilpofika kipindi cha Serengeti fiesta “mwaka huu tutakuwa na Rick Ross na kwamba watanzania waendelee kujenga imani na Serengeti fiesta kwani kila kilele cha tamasha hilo kwa mwaka, ni mwanzo wa maandalizi ya tamasha hilo kwa mwaka unaofuata.
Rick Ross ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaotamba sana katika miondoko ya kurap (hip hop) katika majukwaa ya matamasha mkubwa nchini marekani, atawasili hapa nchini siku ya alhamisi tayari kabisa kutumbuiza katika maadhimisho ya kilele cha tamasha la Serengeti fiesta siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki hii.
Tamasha la Serengeti fiesta linafikia hatua hiyo likitokea nyanda za juu kusini Mbeya na Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wasanii mabali mbali wa miondoko ya bongo flava walishambulia jukwaa kwa nyakati tofauti na kuwatumbuiza vilivyo mashabiki wa tamasha la Serengeti fiesta waliokuwa wamefurika katika viwanja vya sokoine jijini mbeya na Samora mjini Iringa.
Wasanii walioshiriki katika tamasha la Serengeti fiesta nyanda za juu kusini ni pamoja na Inspector Haroun, Juma Nature, Roma Mkatoliki, Linah, Amini, Supa nyota Serengeti fiesta 2012 na wengine.
Mashabiki na wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanatarijwa kuungana pamoja katika viwanja vya leaders kushuhudia shamramshamra na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa kizazi kipya huku wengi wao wakisubiria kwa hamu kubwa kumuona msanii Rick Ross kwa macho yao wenyewe kwa kiingilo cha shilingi za kitanzani elfu 20000/= kwa wale watakaonunua tiketi zao mapema na elfu 25000/= kwa wale watakaonunu tiketi getini.
Tamasha la Serengeti fiesta hufanyika kila mwaka amapo mwaka jana Serengeti fiesta limleta mmoja kati ya wasanii wakubwa nchini marekani Ludacriss ambaye alitumbuiza katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar esSalaam.
 Ajira mbalimbali za muda na za kudumu zimekuwa zikianzishwa kupitia Serengeti fiesta katika maeneo yote ambayo tamasha hilo lilipata kupita zikiwemo kuibuliwa kwa wasanii chipukizi na baadaye kujitegemea kimuziki, kujengeka kwa majina ya wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika zaidi kwa mashabiki wa muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu kupitia tamasha hili la Serengeti fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia ya Serengeti premium lagaer.  

0 comments:

Post a Comment