Tuesday, October 16, 2012

Mr Blue Kuja na 'Nipende Kama Nilivyo'

 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Mr. Blue baada ya kufanya vizuri na ngoma ya ‘Loose Control’, ameamua kuweka wazi kuwa mashabiki wake wasubiri ngoma mpya Nipende Kama Nilivyo’ itakayotoka hivi karibuni audio na video akiwa amemshirikisha producer Man Water.

Msanii huyo alisema kuwa huo ni ujio mpya kabisa na watu wasubiri kuona utofauti katika kazi zake, na kikubwa anachokifanya sasa ni kubadilika katika kila ngoma anayoitoa ili kwenda na wakati pamoja na kuwapa kile wanachokihitaji mashabiki wake.



“Nimemaua kumshirikisha ‘Man Water’ ndani ya ngoma yangu najua watu watashtuka sana kwa sababu hawajawahi kumuona akiimba lakini wategemee ujio mpya kabisa kutoka kwangu, ingawa sihitaji kuongea sana nataka mashabiki wangu waone wenyewe,” alisema.

Mwandishi alipomuuliza
Byser kuhusu kutengeneza albamu kwa ajili ya mashabiki wake, alijibu kuwa hana wazo hilo kabisa katika akili yake kwa sasa kwani anaamini kwa upande wake single ndiyo zinazofanya vizuri kuliko hata albamu huku akiongeza kuwa watu wengi hawana muda wa kununua albamu kutokana utandawazi uliopo sasa ingawa anaamini tabia hiyo ipo kwa Tanzania pekee na si nchi zilizoendelea.
 

0 comments:

Post a Comment