Mrembo Jokate Mwegelo baada ya watanzania wengi kumfahamu kwa kujihusisha
na ishu za urembo, leo mchana ametangaza goodnews kwa kuzindua kampuni yake ya
KIDOTI ambapo pia bidhaa yake mpya ya nywele imezinduliwa.
Ni kampuni ambayo haikua rahisi yeye kuianzisha kutokana na kukatishwa
tamaa, alitamani kuwa na hii kampuni toka miaka minne iliyopita lakini mwaka
jana ndio akapata mtu wa kumsaidia kutengeneza hizo bidhaa ambazo mtaji wake ni
zaidi ya dola za kimarekani elfu thelathini ambazo ni zaidi ya milioni 40 za
Tanzania.
Kabla ya kuanza kuzitengeneza hizi nywele, Jokate ambae ana masters ya
mambo ya siasa alifanya utafiti wa hiyo biashara kwa karibu mwaka mzima, na
sasa zitakua zinauzwa kwenye saluni mbalimbali za kike Tanzania.
Hizi nywele zinatengenezwa hapahapa Tanzania ambapo J amesema sehemu ya
faida yake ataitumia kusaidia wasichana wa Ruvuma ambapo timu nzima ya kampuni
ya Kidoti ni watu sita.
Jokate atasikika kwenye AMPLIFAYA ya Clouds Fm kuanzia saa moja usiku leo
october 10 2012
0 comments:
Post a Comment