
Msanii wa
filamu na muziki wa kizazi kipya bongo Baby
Madaha, yupo katika huzuni kubwa baada ya kumpoteza mama
yake mzazi jana usiku kufuatia kuugua kwa muda mrefu. Mwili wa marehemu
unasafirishwa leo kupelekwa Musoma nyumbani kwao ambapo mipango yote na taratibu
za kuzika zitajulikana huko.
Mwandishi wa
mtandao wa DarTalk, alifika kwenye msiba huo maeneo ya
Kinondoni, na kukutana kuna umati mkubwa wa watu ambao walifulika kumpa
pole msanii huyo ambaye ni kipenzi cha watu.
Hata hivyo
mwandishi wa habari hizi, alizungumza na Madaha
ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema
kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu
vingi ndani ya maisha yake.
“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu
kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele
za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko makubwa sana.
0 comments:
Post a Comment