Msanii Farid Kubanda, ‘Fid
Q’ a.k.a Ngosha ze Swagga Don, ametoa ushauri kwa wasanii wanaotaka umaarufu
wasijifananishe na wale waliotangulia katika sanaa hiyo muda mrefu.
Akizungumza kwa hisia,
Fid alisema wapo wasanii wazuri tu, lakini uwezo wao unashuka kutokana na
kuanza kusimama kwa kujifananisha na wakongwe walioanza kusota muda mrefu.
Alisema wasanii
wakongwe tayari wana mtaji mkubwa wa mashabiki, hivyo kamwe hawataweza kupondwa
au kuonekana vituko kwasababu ya wasanii wachanga wanaoingia na kutoka.
“Wasanii wachanga
wakaze buti, lakini wasidharau kaka zao, maana tayari hao wana mtaji mkubwa wa
mashabiki, hivyo hawawezi kuwa kama wao"...
“Wakifanya hivyo
wataanguka na kupoteza thamani yao, maana Fid Q nimeanza kitambo na uwezo wangu
umeshaonekana kuwa ni mkali na naweza kuhimili vishindo vya muziki wa Hip Hop
nchini,” alisema Fid Q.
Fid Q ni miongoni mwa
wasanii wanaofanya vyema katika tasnia ya muziki wa Hip Hop nchini, akiweza
kukaa kileleni kwa miaka mingi sasa.
0 comments:
Post a Comment