Mashindano ya Redds Miss Tanzania kwa
sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda
ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla ya 30 .
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es
Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga
alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio
makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa
hali ya Juu.
Washiriki wengi wa
mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na
wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa
katika shindano la mwaka huu.
Baada ya kukamilika kwa
mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30
walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012
wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya
kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao
watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda
kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA
2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa
Hotel ya Blue Peal (Ubungo
Plaza).
Kwa Upande wake Meneja
wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu
wa Redds Miss Tanzania
wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa
tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa
kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa kuzingatia
mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania
atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti katika
Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao. 2013.
0 comments:
Post a Comment