Showing posts with label Zanzibar. Show all posts
Showing posts with label Zanzibar. Show all posts

Monday, December 30, 2013

Ufunguzi wa Jengo jipya la kiwanda cha uchapaji


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja,ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea jengo jipya la kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,kuhusu mashine mpya zilizonunuliwa na idara ya uchapaji,wakati alipotembelea kuangalia mashine kuona utendaji wake kazi,baada ya kufanya unguzi rasmi,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiuliza suala kwa Mkurugenzi Kanda wa Kampuni ya MFI DOCUMENT SOLUTION LTD, Rama Subramanian,ikiwa ndio wataalam wa mshine za uchapishaji,alipotembela na kuona zinavyofanyakazi,wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda hicho,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa mashine ya CTP,ambayo inatoa picha kwa kutumia Plat,Mohamed Abass Rajab,(wa tatu kushoto) wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda cha Uchapaji cha Zanzibar jana,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Wednesday, June 26, 2013

ZANZIBAR WAZINDUA KONGAMANO LA KUKABILIANA NA MAAFA

Imeelezwa kuwa Zanzibar inaweza kukumbwa na Janga la uhaba wa Maji  ifikapo mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo watu kuharibu Vyanzo vya Maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud ameeleza hayo alipokuwa akizindua Kongamano la Kitaifa la kukabiliana na Maafa lililofanyika Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Amesema kuna Tafiti zimefanywa  na kuonesha hatari inayoikabili Zanzibar katika upatikanaji wa Maji na kwamba juhudi binafsi zinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo.
Aboud amesema Wasomi na Wataalam kwa ujumla wanapaswa kufahamu hali hiyo na kuisaidia Serikali katika kukabiliana na Upungufu huo badala ya kukaa kimya na kulaumu.
“Wasomi wamekaa kimya sana hawatoi ushauri wa kitaalamu kwa Serikali juu ya nini kifanyike ili kuijengea uwezo Serikali na Jamii kwa ujumla kukabiliana na Majanga ” Alifafanua Aboud.
Ametolea Mfano wa Zao la Nazi linavyoendelea kupotea katika Visiwa vya Zanzibar na kusema kuwa Wataalamu wameshindwa kuja na namna bora ya kupata Minazi bora  inayozalisha zaidi na kuchukua eneo dogo kuliko Minazi iliyopo.
Aidha Waziri Aboud amesisitiza  Idara ya Maafa kwa kushirikiana na wadau wengine  kuendelea kutoa Elimu ya kukabilaiana na Majanga  kwa jamii ili kupata jamii salama.
“Ndugu wadau Elimu ni Muhimu kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini hadi juu,kwa kukosekana Elimu ya Majanga baadhi ya wakati hata Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanakuwa wagumu kupitisha Vifungu vya Bajeti za Idara,yote ni kiashirio cha uelewa mdogo juu ya Majanga” Aliongezea Aboud.
Awali akimkaribisha Waziri Aboud, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa alisema licha ya kukabiliwa na Changamoto mbalimbali Idara yake imejipanga vyema kuhakikisha inafanya majukumu yake ya msingi ikiwemo kukabiliana na Maafa.
Amesema kwa Sasa Idara ya Maafa ina mpango wa kuainisha maeneo hatarishi katika Ramani  ili kusaidia ufahamu na namna ya kuweza kukabiliana na maafa pale  yanapotokea.
Kongamano hilo la kitaifa la kukabiliana na maafa limendaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  ambapo kwa siku mbili Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi watajadili na namna bora ya kukabiliana na Majanga Zanzibar.
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 26/06/2013