Hit maker wa Mawazo, Mbagala, Kamwambie na sasa
My Number, Diamond Platnumz ametangaza fursa ya ajira kwa vijana wenye uwezo na
elimu ya ku-shoot na ku-edit videos.
Mpango huu unawahusu vijana wenye uwezo wa
kutumia kamera zote ikiwa ni za zamani na sasa, pia kuwa na sampuli za kazi zao
walizowahi kufanya.
Vigezo vingine ni pamoja na kuwa sampuli hizo
kuwa na quality ya kuanzia 1080 na kuendelea, pia kwa kijana anayehitaji nafasi
hiyo anatakiwa kuwa na umri wa miaka kuanzia 20 hadi 35.
Aidha anatakiwa kuwa mbunifu na awe tayari
kusafiri popote duniani na kwa wakati wowote. Amewataka kwa walwe wote
wanaoamini wana sifa hizo wawasiliane nae kwa Email Address; diamondplatnumz@gmail.com
au simu
+255755700400.... Kumbuka,
uwe unaisha Dar-es-Salaam...!