Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limewasilisha malalamiko kwa serikali ya Urusi baada ya wandishi wake wa habari kushambuliwa Kusini mwa nchi hiyo.
Baada ya kuwaarifu maafisa wa huduma ya dharura , waandishi hao walipelekwa katika kituo cha polisi na kuhojiwa kwa saa nne.
Picha walizokuwa wamenasa kwenye kamera zilifutwa wakati wakiwa kwenye kituo cha polisi.
BBC inasema kuwa imechukizwa na kitendo hicho na kutoa wito kwa maafisa wa utawala nchini humo kuchunguza taarifa hizo pamoja na kuwataka kulaani kitendo hicho.







0 comments:
Post a Comment