IMEELEZWA kuwa pombe inaua watu milioni 3.3 kila mwaka
duniani kote, ikiwa ni zaidi ya Ukimwi, Kifua Kikuu pamoja na magonjwa mengine,
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa hiyo siku ya Jumatatu na kuonya kuwa
unywaji wa pombe na matumizi ya kilevi yanazidi kuongezeka.
“Hii kwa kweli inamaanisha kuwa kila ndamni ya sekunde
10 kuna kifo kinatokea,” Shekhar Saxena,
ambaye ni mkuu wa Idara ya magonjwa ya Akili na madawa ya kulevya wa WHO, aliwaambia
waandishi wa habari Jijini Geneva.
Matumizi ya kilevi yalisababisha vifo milioni 3.3 kwa
mwaka 2012, ambapo WHO wamesema kuwa ni sawa na asilimia 5.9 ya vifo vyote
(asilimia 7.6 kwa wanaume na 4.0 ni
wanawake)
Ikilinganishwa na HIV/AIDS ambayo inaua kwa asilimia
2.8, Kifua Kikuu kinasababisha vifo kwa asilimia 1.7 na magonjwa mengine kwa
asilima 0.9, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa.
"Mbinu za ziada
zinahitajika kuwalinda watu kutoka athari za matumizi hasi ya pombe kwa afyaMahitaji,”
Oleg Chestnov ambaye ni daktari wa Shirika hilo alisema katika taarifa yake
wakati wa uzinduzi wa utafiti wa ripoti kubwa juu ya matumizi ya pombe na madhara
yake kwa afya ya umma.
Matumizi mabaya ya pombe
huwafanya watu kuugua magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani, kifua kikuu, HIV na
Pnemonia, ilieleza taarifa hiyo.
Vifo vingi vinavyotokana na matumizi ya pombe, karibu
robo tatu husababishwa na magonjwa ya moyo na kisukari.
Ulevi wa pombe kupindukia na kuharibu afyav
unakadiriwa kuwa ni asilimia 16 katika dunia nzima.
Wakati watu katika
mataifa tajiri zaidi duniani , katika nchi za Ulaya na Marekani, n wanyawaji
kuliko watu walioko katika nchi masikini bado hali ya uchumi wao inaonekana
kupanda na hivyo kusababisha matumizi ya pombe kuongezeka.
Lakini mbali na kila mtu duniani
kuwa mlevi, inaelezwa karibu nusu ya watu wazima wote duniani kamwe hawajagusa
pombe na karibu asilimia 62 walisema hawajagusa wala kunywa kwa mwaka uliopita,
ripoti hiyo ilionyesha.
Chanzo Daily Nation







0 comments:
Post a Comment