Friday, February 28, 2014

CHADEMA YAENDELEA NA KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGO MKAONI IRINGA

 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo jana.
 Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
 Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.
Mgombea  wa CHADEMA akipokelwa Lumuli;

0 comments:

Post a Comment