Juan Mata.
MANCHESTER United
imekubali kulipa ada ya pauni milioni 37 ambayo ni rekodi kwa klabu ili
kumnasa Juan Mata kutoka Chelsea na hii inasaidia kidogo kupoza
machungu ya kutolewa Capital One Cup.
Bosi
wa Chelsea Jose Mourinho ameidhinisha dili hilo baada ya mazungumzo na
maofisa wa klabu na sasa Mata anategemewa kufanya vipimo vya afya jijini
Manchester kesho Alhamisi.
Mtendaji
mkuu wa Manchester United amekubali kuvunja rekodi ya klabu ya usajili
kwaajili ya Mata ili kuokoa msimu unaokwenda kombo kwao.
Vipigo
saba katika Ligi Kuu ya England vimeiacha United ikiwa nyuma kwa pointi
6 kutoka nafasi ya nne kwanye msimamo wa Ligi ambayo ingewawezesha
kushiriki Champions League msimu ujao – lakini kuongezeka kwa Mata
kunatarajiwa kuleta uhai mkubwa.







0 comments:
Post a Comment