Rais
Jacob Zuma ametangaza muda mfupi uliopita kwamba mazishi ya Nelson Mandela
yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu, katika jimbo la
Eastern Cape.
Rais
Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu
mlingoti katika muda wote huo.
Aidha
ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya
maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa
kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani,
mstaafu Bill Clinton na Waziri Mkuu wa UingerezaDavid Cameronni baadhi ya
viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.
Sala
ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013
jijini Johanesburg.
Mwili
wake utawekwa katika jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba
11 hadi 13 kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kabla ya kupelekwa kijijini
Qunu kwa ajili ya mazishi.
Uwanja
wa Taifa wa michrezo wa FNB ambako sala rasmi ya Kitaifa ya mazishi itafanyika Desemba
10, 2013

Jengo
la Union Buldings ambapo mwili wake utawekwa hapa kwa ajili ya kupewa heshima
za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013.
Ulinzi
mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake QUnu ambapo atapumzishwa
katika nyumba yake ya milele Desemba 15,2013.







0 comments:
Post a Comment