Thursday, December 5, 2013

Cristiano Ronaldo kuzindua jumba lake la Makumbusho?

ronaldo 5
Imefahamika kwamba December 15 2013 ndio Cristiano Ronaldo ambae ni mchezaji wa Real Madrid anafungua jumba lake la kumbukumbu ambalo litakua na vitu mbalimbali vinavyohusu kazi yake ya soka na maisha yake.
Jumba lenyewe la makumbusho litakua nyumbani kwao kwenye kisiwa cha Madeira ambapo kujengwa kwa jumba hili haimaanishi ndio anastaafu soka hivi karibuni.
Unaambiwa jumba hili la makumbusho halitamnufaisha Ronaldo mwenyewe bali hata uchumi wa kisiwa hiki utaongezewa mapato kutokana na pesa ambazo watu mbalimbali watakua wanalipa kila wanapotembelea, kwenye hii Idea iliyotoka kwa Ronaldo na mama yake mzazi ni kwamba mapato yatakayotokana na kiingilio yatakwenda moja kwa moja kwenye mamlaka husika za mapato za kisiwa hiki.
Imefahamika pia kwamba huu ni mwanzo tu wa safari ya Ronaldo anaetaka kuwekeza kwenye sehemu nyingine nyingi za Madeira.
ronaldo 6 
SOMA ZAIDI: Millardayo

0 comments:

Post a Comment