
Katika habari zote hizo zimelihusisa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari hizo.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa hizi:
(i) Shirika la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini ripoti iliyotajwa katika
habari hizo kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
(ii) Shirika husimamia shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi
za Taifa pekee kiutendaji, ambapo baadhi ya maeneo yaliyotajwa
Katika habari hizo kama Selous na Liwale kiutendaji hayapo ndani
ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
(iii) Kama Shirika la Umma, hufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na
kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola katika kushughulikia uhalifu wa
aina mbalimbali ikiwemo ujangili.
Ni kwa mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki
na taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa
kufanyia kazi.
Tunachukua nafasi hii kuviomba vyombo vya habari kushiriki katika juhudi
za kupambana na ujangili kwa kuwa waangalifu katika kuandika habari za
kutuhumiana kabla ya kuwa na ushahidi kamili ambao ni haki ya kimsingi
ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.
Imetolewa na Idara ya Uhusiano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
07/10/2013
0 comments:
Post a Comment