Meneja Rasiliamali watu kutoka Kampuni ya Bima ya Jubilee bi. Gloria Ngasa akiungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa mawakala wa bima uliofanyika katika Hotel ya New africa jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kutoa elimu ya kutosha na yenye tija kwa ili jamii iweze kutambua umuhimu wa kujikatia baima za aina mbalimbali mfano za moto, afya, magari, na vyombo vingine vya moto ili endapo itatokea kitu chochote bima zao ziweze kuwasaidia
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Jubilee Bw. George Alande akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Mkutano huo wa mawakala wa bima wanaofanya kazi kwa kushirikiana na Jubilee wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu bima mbalimbali na faida zake iliyofuatiwa na hafla fupi yakuwakabidhi zawadi baadhi ya wakala hao ikiwa ni sehemu ya shukrani na kutambua utendaji wao mzuri.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Jubilee Bw. George Alande (mwenyesuti)akikabidhi zawadi Mkurugenzi wa kampuni ya bima ya Venture Bw. Alex Lemnge (kulia)ambapo pia ni washindi wa kwanza kati ya mawakala waanaofanya kazi kwa kushirikiana na kampuniya bima ya Jubilee.
PICHA NA PHILEMON SOLOMO WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment