Tuesday, October 15, 2013

Kala Awapa Big Up Fans Wake, Alamba Mkataba Mnono wa Pepsi

Balozi mpya wa kinywaji baridi cha Pepsi, Kala Jeremiah amesema juhudi zaidi ndiyo zimeweza kufanikisha mpaka yeye kufikia hatua ya kukubalika na kampuni hiyo na kusaini mkataba mnono wa kuwa balozi wa kinywaji hicho.
Kala alifunguka kinamna kwenye 255 ya XXL ya Cloud Fm jana, ambapo alisema licha ya juhudi zake lakini pia mashabiki wake wamekuwa ni mchango mkubwa katika kufanikisha kupata mkataba huo.
"Unajua hata wao (makampuni) wanapoangalia huwa hawachukui mtu kwa kuangalia kile unachofanya tu, huwa wanaangalia pia jamii inakukubali vipi na wewe mwenyewe unajiheshimu kiaje, so katika hilo nashukuru mafans wangu ambao wamekuwa wakinikubali muda wote" alisema kala.
Aidha Kala amesema pia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vimekuwa mbele kumpigania  kuhakikisha kuwa anafahamika katika jamii  na kampuni kubwa kama hizo.
Hata hivyo kala alikataa kutaja kiasi cha fedha anacholipwa baada ya kusaini mkataba huo.



0 comments:

Post a Comment