
zikiwa zimepita siku 30 tangu msanii anae fanya poa na single yake
"jambo jambo" Steve R&B kuweka wazi kuwa, hajawahi kuwa na mkataba
na producer wake Man Walter, wa kusimamia kazi zake, ikiwa ni baada ya
kampuni inayomsimamia kazi zake "Kvelli", kushangazwa na kumsikia
producer Man Walter ambae alisikika akijinadi kuwa ndio msimamizi wa
kazi za Steve.Leo hii kupitia XXL amefunguka na kusema kuwa, alikuwa
akifanya kazi na Steve na walikuwa na mkataba wa maneno.
"kosa langu kubwa ambalo huwa nalifanya, kwasababu sio mara ya kwanza,
ni kukaa na msanii, unajua saa ingine msanii anakuja, unampa bei zetu za
studio, lakini anakua hawezi kulipa, so inabidi tufanye mkopo, yaani
mkopo kwa maana nitaanza kumtengeneza na kahakikisha kazi zake
zinasambaa kote ili mwisho wa siku na mimi niweze kurudisha changu, sasa
tukiwa katika maongezi hayo, ndio hapo ambapo tunakua hatuchukulii
serious na kuandikishana mikataba, yaani unaona kama jamaa hawezi kuja
kukuzunguka, lakini misho wa siku akikuzunguka ndio hivyo tena unakuwa
huna ushahidi" amesema Walter.
Licha ya kusifia jinsi ambavyo wimbo wa jambo jambo unavyofanya poa
katika station mbali mbali, Walter leo ameachia wimbo wenye beat
(riddim) sawa na ya jambo jambo inayoitwa "NAWAOGOPA" akiwa ameimba na
kuproduce mwenyewe ikiwa ni maalum kwa ajili ya mahaters
nilipomuuliza kama ni mahususi kwa ajili ya Steve, walter alisema hapana ni kwa ajili ya wote ma haters tu.
pata kuisikiliza hapo chini
0 comments:
Post a Comment