Peter Ash akikabidhi Cheti kwa Mmoja
wa wahitimu katika Hafla hiyo.
Shirika lisilo la Kiserikali la kutetea
watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) Under The Same Sun (UTSS)
limetoa Vyeti kwa walemavu wa Ngozi 43 waliohitimu ngazi mbalimbali
za Elimu kwa kusomeshwa katika vyuo mbalimbali na Shirika hilo.
Akizungumza katika Hafla ya Utoaji wa
Vyeti hivyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,
Mwenyekiti wa IPP Bw Reginald Mengi ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi,
amewapongeza wahitimu hao kwa kuhitimu na kuwataka kujiamini na kuamini kuwa na
wao wanaweza wakiwa mahali popote.
Bw, Mengi pia amewapongeza sana Shirika
hilo kwa kuwasomesha walemavu wa Ngozi kwani wamewapa ujasiri wa kujiamini kuwa
wanaweza kufanya lolote katika jamii na jamii ikawakubali.
“Unatakiwa ujikubali kuwa nawewe
unaweza na unaweza ukawa namba moja kati ya watu wengi, binafsi nawapongeza
sana UTSS kwa kuwawezesha walemavu wa Ngozi kupata Elimu bora “amesema Dk
Mengi.
Katika Warsha hiyo iliyofanyika leo
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Baadhi ya Makampuni ilijitolea
kuajiri wahitimu 20 ambao walikuwa tayari kupata Ajira kwani wengine waliopata
vyeti bado wanaendelea na masomo yao.
Aidha, Muasisi wa Shirika hilo Peter
Ash, alielezea changamoto mbalimbali na jinsi Albino wanavyohitajiwa kusaidiwa
na kupewa nafasi katika jamii. Alisema wahitimu hao watakuwa ni mfano kwa watu
wengine kuonyesha kuwa ikiwa watawezeshwa nao pia wanaweza.
Wahitimu wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
na Mgeni Rasmi pamoja na Uongozi wa UTSS.
Mkurugenzi na Muhasisi wa UTSS Canada
na Tanzania Bw Peter Ash akiwapongeza wahitimu katika Hafla hiyo.
Waajiri kutoka katika Makampuni
mbalimbali waliojitolea kuwa ajiri wahitimu hao
Mwanamuziki mlemavu wa Ngozi Ras Six akitoa
Burudani katika Hafla hiyo
0 comments:
Post a Comment