Song: Wazo La
Leo
Artist:
Stamina Feat Fid Q
Studio: Bongo
Records
Producer: P
funk Majani
Song
Writters: Stamina (verses) & Fid Q (chorus)
Intro...
U know what
majani??nice to meet you homie
Its moro town
baby,,,shorobwenzi
Verse 1.
(Stamina)
Elimika
nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi
la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo
Vaa
uaminifu,tupa boksi la kondomu
Hip hop
haijengwi na bifu,underground usijaze fomu
Maisha ni
kujipanga, mganga usigawe irizi
Viongozi
msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina
kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi
shamba,dec mbegu siku hizi hazioti
Maisha njia
panda,mtembezi chagua pa kwenda
Uchumi vazi
la bwanga,ukishuka uvishe suspenda
Shiba kwa
nia,ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we
shukuru ukifaulu kila tendo
Punguza
pupa,mpendaji uingie ndoani
Mapenzi
yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani
Usilale
kijinga,kwenye kitanda cha ushamba
Unaweza kuwa
shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga
Chorus. (Fid
Q)
Hiki kijiko
unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu
usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la
kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge
la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo
wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe
nasaha.
{hilo ndo
wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
Verse 2.
(Stamina)
Underground
panga tenzi,ustar hauji kwa promo
Hakuna tajiri
wa mapenzi,kapuku punguza ngono
Bora uitwe
mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba
Mapenzi
yakikusumbua,tafuta daktari wa kitanga
Vazi
unaloishi,mwenyezi yeye ndio disegner
Shetani
akikushawishi, mvute kwake kama dayna
Dunia
duara,jitahidi uizunguke
Mla bata
starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke
Huna undugu
na bakhersa,niaje aje unakula unga
Mateja
wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda
Dogo
jifunze,heshima sio upaparazi
Mwambie na
dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi
Kama unajijua
ni mchoyo,basi usingoje kupewa
Tafuta pesa
kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe
salamu,the great braza kanumba
Mwambie bongo
sio tamu,na lulu bado wamemfunga
Chorus(fid q)
Hiki kijiko
unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu
usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la
kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge
la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo
wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe
nasaha.
{hilo ndo
wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza
Nchi tayari imekonda,mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri,jipange kuikwepa hasara
kijana vazi la msuli,haliwezi kukuvisha busara
ukiishi kwa hisia,kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia,ujivue kuwa mtanza
kata ya kijiji,haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji,msuli ukishuka kimeo
uchumi umeshika tama,kwenye shavu la mlanguzi
raia usilaumu chama,shiriki kwenye uchaguzi
unaweza ukavaa kinga,ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga,sambaza ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa,ukiwa nae fanya vya maana
akiondoka atakutesa,utamsaka usiku na mchana
Chorus. (Fid
Q)
Hiki kijiko
unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu
usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la
kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge
la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo
wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe
nasaha.
{hilo ndo
wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
0 comments:
Post a Comment